Show Za Diamond Zinajazwa na Wazungu na Wajamaica Sio Waafrika Pekee- Babu Tale

Meneja wa staa wa Muziki wa Bongo fleva nchini Diamond Platnumz, Babu Tale amefunguka na kueleza hali ya shoo za Diamond kwenye Tour ya ‘A boy from Tandale’ inayofanyika nchini Marekani.

Babu Tale amefunguka na kuweka wazi kuwa katika shoo zinazoendelea kufanyika nchini Marekani kwa sasa zinakuwa zinahudhuriwa na mashabiki wa mataifa mbali mbali kama wazungu na sio Waafrika tu kama ilivyozoeleka.

Kwenye mahojiano aliyofanya na JJ wa Jembe FM Babu Tale ambaye ameongozana na Diamond katika tour hiyo, amesema kuwa show za Diamond zimekuwa ni za watu wote na si wale kutokea Afrika pekee.

Ukiangalia clip ambayo ameposti Diamond utaona watu weupe kibao, nimeona wazungu kibao, Jamaica walikuwepo“.

Imekuwa ni Kasumba kuwa wasanii wanaoenda kufanya shoo nje ya nchi huishia kupiga shoo za sebuleni jambo ambalo Diamond amekuwa akilibadilisha kwani amekuwa akionekana akipiga shoo Kwenye kumbi kubwa na kujaza mashabiki kibao.

Jumba La Mobetto Alilozawadiwa na Diamond Lagubikwa na Utata

Wiki iliyopita habari zilienea Kwenye mitandao ya kijamii kuwa Diamond amemnunulia mjengo wa fahari mama mtoto wake na Hamisa Mobetto ambapo Mama Mobetto alithibitisha taarifa hizo.

Lakini hivi sasa Global Publishers wanaripoti kuwa Habari hiyo siyo ya kweli kwani kwa taarifa waliyokuwa nazo ni kuwa nyumba ile haijanunuliwa bali imepangishwa tu kwa muda.

Baada ya Tetesi hizo gazeti hilo lilienda kufanya uchunguzi ambapo Jirani mmoja wa Mobeto aliyeomba hifadhi ya jina, alipoibukiwa na wanahabari wetu, aliweka wazi kuwa nyumba hiyo hajanunuliwa na ameshangazwa na habari kwamba amenunuliwa.

Kwa kweli nimeamini hawa mastaa wanapenda kujikweza, yaani nyumba hii tumeona mchakato wote na mwenye nyumba tunamjua lakini mitandaoni tunaona mama Mobeto anasema Diamond kawanunulia”.

Lakini baada ya taarifa hizo gazeti hilo lilimsaka mmiliki wa mjengo huo ili aweze kuthibitisha taarifa hizo ndipo ndugu wa mmiliki alipofunguka:

Mimi mwenyewe niliona kwenye mtandao kwamba wamenunua, nikashtuka sana ikabidi niende kumuonesha babu (mmiliki), akasema si kweli ndipo wakapuuza tu maana“.

Mama mzazi wa Mobetto anayejulikana kama Shufaa Rutiginga aliweka wazi Kwenye mahojiano na Wasafi Tv kuwa Diamond alinunua mjengo huo maalumu kwa ajili ya mtoto wake Dyalan.

Harmonize Atangaza Ujio Wa Albamu Yake

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB, Harmonize ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Kwangaru’ ametangaza ujio wa albamu.

Harmonize ametangaza Habari hiyo njema kwa mashabiki zake wanaopenda muziki wake kwani hiyo ndio itakuwa albamu yake ya kwanza tangu aanze kufanya Muziki.

Kwenye Interview yake na Bongo5, Harmonize amefunguka kuwa analazimika kutoa albamu kwa sababu ndio utambulisho rasmi wa msaniii ndani ya tasnia ya muziki.

Nipo ndio nashughulikia albamu yangu lakini nipo kwenye hatua za mwisho sana, so muda wowote naweza kuitangaza lini itatoka, itakuwa na wasanii tofauti tofauti“.

Siku za nyuma Diamond Platnumz alishawahi kufunguka kuwa wasanii wote wa WCB wanatoa Albamu zao kwa muda fulani ambapo yeye ameshatoa albamu yake ya ‘A boy from Tandale’.

 

“Siwezi Kuingilia Mahusiano Ya Diamond”-Mbosso

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB, Maromboso almaarufu kama Mbosso ameweka wazi kuwa hawezi kuingilia Mahusiano ya Bosi wake Diamond Platnumz.

Diamond ambaye ni Mkurugenzi wa label ya WCB amekuwa kivutio sana Kwenye mitandao ya kijamii hasa linapokuja suala la Mahusiano Yake binafsi na Familia yake.

Mbosso ambaye alijiunga Rasmi WCB Miezi michache iliyopita amefunguka na kusema hawezi hata siku moja kuingilia Mahusiano binafsi ya Diamond.

Suala hilo liliibuka Kwenye mahojiano aliyokuwa anafanya na Sam Misago Tv, ambapo aliulizwa kama anaweza kumpa ushauri gani Diamond hasa linapokuja suala lake la Mahusiano.

Mahusiano Yake bwana Chibu daaah siwezi kumuingilia huko! Naomba niishie hapa siwezi kuingilia mahusiano yake, Unajua ndio displini niliyojiwekea kuna vitu naweza kuviingilia na kuna vitu siwezi kabisaa”.

Mapema mwaka huu mpiga picha maarufu wa Diamond anayejulikana kama Kifesi alifukuzwa kazi baada ya kuingilia Mahusiano ya Diamond baada ya kumshauri arudiane na Zari badala ya Hamisa.

Diamond Platnumz Apata Ajali Ya Gari Nchini Marekani

Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz alipata ajali siku chache zilizopita alipokuwa nchini Marekani alipoenda kufanya shoo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond alisema alipata ajali hiyo alipokuwa anatoka kwenye shoo yake usiku wa manane.

Dah Tumepata ajali na kunusurika kufa usiku wa leo wakati tunatoka kwenye show….ila Mwenyez Mungu ametupa nafasi nyingine tena ya kuishi na kuendelea kushikana mkono na vijana wenzangu mtaani kwa pamoja tuziokoe familia zetu duni??….”.

Diamond alipata ajali siku chache zilizopita nchini Marekani alipoenda kufanya shoo ya tour yake ya   ‘A boy from Tandale’ Lakini haraka aliweka wazi kuwa hajaumia.

Mbosso- Nyimbo Zangu Hazipigwi Redioni

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva kutoka label ya WCB Maromboso au maarufu kama Mbosso ameongelea Kitendo Cha nyimbo zake kutopigwa na baadhi ya media.

Mkurugenzi wa WCB Diamond Platnumz amekuwa kwenye mgogoro na baadhi ya vyombo vya habari hadi kupelekea nyimbo zake kufungiwa na vituo hivyo.

Wasanii wote ambao wako chini ya WCB wamekuwa wakibaniwa nyimbo zao kupigwa Kwenye Media hizo na Mbosso akiwa mmoja kati ya wasanii hao.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Mbosso ameweka wazi kuwa ingawa  nyimbo zake hazipigwi na baadhi ya media lakini anashukuru zinadai kila vyema kwa mashabiki zake.

Ukizungumzia moja ya wasanii ambao hawakupata bahati ya kupata nafasi kubwa kwenye radio station, mimi pia naweza kusema nipo.

Sikupata bahati kabisa nyimbo kupigwa kwenye radio station lakini wananchi wamenipokea, wamesema Mbosso tunakusapoti, wamenisapoti nashuru leo nimefika nilipofika”.

Baada ya media zaidi ya nne kugoma kupiga nyimbo za Diamond na wasanii wote wa WCB, Diamond alifikia uwaumuzi wa kufungua Stesheni yao ya Wasafi Tv.

Mr. Blue Awainulia Mikono Ali Kiba na Diamond

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Khery Sameer  au maarufu kama Mr. Blue amewainulia mikono mastaa wa Bongo fleva Diamond na Ali Kiba.

Mr. Blue amefunguka na kuweka wazi kuwa anaona kabisa kuna vitu vya Ziada vinavyowafanya Ali Kiba na Diamond wazidi kupata mafanikio katika tasnia hii.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Mr Blue amesema wanamuziki wengi chipukizi hutamani kuwa kama wawili hao bila kufahamu mbali na kufanya muziki wanajituma, wana nidhamu na wana malengo ya kufika

Unajua wengi hutamani kuwa kama fulani kwenye muziki hasa watu wanaofanya vizuri zaidi kwa sasa kama Diamond na Kiba, lakini bila kufahamu kwamba ili ufanikiwe ni lazima uwe na vitu vya ziada mbali na kuimba kawaida.

Kwa ushauri wangu, wanamuziki chipukizi waangalie ni vitu gani vya ziada wanavyo wanamuziki wanaotamani kuwa kama wao wavifuate na wataweza kufika kule wanako kuhitaji”.

Ni wiki chache tu zilizopita Mr. Blue alikana taarifa za  kuwa ana bifu na Diamond baada ya tetesi za muda mrefu zilizodai hivyo.

Baba Diamond na Baba Ommy Dimpoz Warushiana Maneno

Baba mzazi wa Staa wa Bongo fleva Ommy Dimpoz,  Mzee Faraji Nyembo amemtolea povu Baba wa staa Diamond Platnumz, Mzee Abdul Juma kutokana na tabia yake ya kumsema mwanaye vibaya.

Gazeti la Risasi Mchanganyiko  linaripoti kuwa Kwenye mahojiano waliyofanya na Baba Ommy Dimpoz alitoa taarifa ya mtoto wake kuendelea vizuri na kusisitiza hata kama mtoto wake hamsaidii kwa lolote maishani lakini hawezi kumsema vibaya kama Baba Diamond anavyofanyaga kwa mwanaye.

Unajua mimi ni mzazi wa tofauti sana, siwezi kumlalamikia au kumsemea mabaya mwanangu kwenye vyombo vya habari kama anavyofanya baba Diamond, ninachofanya huwa namuombea mwanangu awe na maisha mazuri maana nikimuombea mabaya anaweza kupoteza dira ya maisha yake nitakuwa nimefaidika na nini.

Namshauri baba Diamond awe anamuombea mwanaye mafanikio, aungane naye wawe kitu kimoja, afurahie mafanikio yake ipo siku Mungu atamrudisha kwake amsaidie na siyo kumzungumzia maneno ya kumlaani na kumlalamikia kila siku.

Aige mfano wangu maana mimi huwa simlazimishi mtoto anisaidie bali huwa napambana na hali yangu kwa kufanya kazi kwa bidii na ninampenda sana mwanangu Dimpoz na siwezi kumlaani au kumlaumu maana jina nililompa la Omary ni la baba yangu inakuwaje sasa nimlaani ni sawa na kumlaani baba yangu”.

Baada ya povu hilo gazeti hilo lilimsaka Baba Diamond na kumuhoji kuhusu kile alichosema Baba Dimpoz na alimwaga povu hili:

Sitaki shobo, huyo baba Dimpoz simfahamu kama hana la kuongea anyamaze, amzungumzie mwanaye hata kama niliongea kuhusu Diamond si mtoto wangu yeye inamuhusu nini?”.

Kuhusu huyo Diamond sihitaji kuzungumza chochote kuhusu yeye wala watoto wangu maana hawana faida yoyote kwangu kwa sasa”.

 

WCB Wagoma Nyimbo Zao Kupigwa na Habari Zao Kuripotiwa na Baadhi Ya Media

Label au kundi linalofanya vizuri hivi sasa nchini WCB linaloongozwa na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz limetoa tamko rasmi la kuwataka baadhi ya media wasipige nyimbo zao.

Meneja wa label hiyo Babu Tale ametoa tamko hilo jana wakati akichonga na waandishi wa habari Kwenye uzinduzi wa Wasafi Tv Kwenye king’amuzi cha Startimes.

Babu Tale amevitaka vyombo vilivyokataa kupiga nyimbo zao Mwanzoni viendelee hivyo hivyo na hata visijaribu kuripoti taarifa zao.

Tunaendelea kuwaomba waendelee kushinikiza wafanyakazi wao wasipige nyimbo zetu.

Hatutaki kuona wanapiga nyimbo zetu wala kutoa habari zetu kwa sababu wao walitukataa mwanzo, tunawakataa kwa sababu wao walitukataa“.

Diamond amekuwa katika mgogoro mzito na Media mbali mbali ambazo zimekuwa hazipigi kabisa nyimbo zake ambazo ni Clouds Media na hata East Africa Radio na Tv.

 

Zari Sio Chanzo Cha Diamond Kukonda, Babu Tale Ataja Sababu Hizi

Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz ambaye pia ni CEO wa WCB amekuwa kwenye headlines sana na moja kati ya vitu vinavyo trend ni mwili wake kuisha.

Baada ya Diamond kuonekana anapungua mwili kwa kasi habari zilisambaa Mtandaoni kuwa kisa ni Zari ambapo ilidaiwa baada ya kumwagwa na Zari Diamond alipata mawazo sana na hata kudaiwa eti sahivi hapati matunzo aliyokuwa anapata wakati yupo na Zari.

Lakini Meneja wa Diamond, Babu Tale amefunguka na kuweka wazi kuwa sababu za Diamond kupungua mwili kwa muda mfupi kuwa ni kukosa muda wa kulala kutokana na jukumu zito la ujio wa Wasafi TV.

Kuna baadhi ya watu wanasema msanii wangu anapungua mimi na nenepa navimba, Kama hamjui Media sio kitu kidogo, wakati tunaanza tulijua ni kazi ndogo, kwa miezi sita non stop msanii wangu analala masaa mawili tu, kwa sababu ya kuandaa hiki mnachokiona machoni mwenu.. Wiki mbili za mwanzo tukawa tunakasirika kwa nini anafanya kazi ngumu, ilipofika mwezi tukawa tunaona  ana-loose weight (kupungua uzito) na bado kazi zinaendelea tukawa tunashangaa ana nia gani huyu”.

Lakini pia mwana Familia wa Diamond mwenyewe,ambaye ni dada yake Esma aliwahi kunukuliwa akisema kaka yake kapungua kwa kumiss penzi la Zari.

Uzinduzi wa Wasafi Tv Kwenye Startimes (+picha)

Msanii wa Bongo fleva na CEO wa WCB Diamond Platnumz ametangaza rasmi kuingia ubia na king’amuzi cha Startimes ambacho kitarusha matangazo ya Wasafi Tv.

Siku ya jana Diamond Kupitia ukurasa wake wa Instagram alitangaza kuwa atakuwa na mkutano na waandishi wa habari katika hoteli ya Slipway siku ya leo saa tano asubuhi.

Diamond amezindua rasmi Wasafi Tv ndani ya Startimes Tanzania Bara na visiwani ambayo itakuwa inaruka Live Kupitia chaneli namba 444 katika king’amuzi hiko.

Wasafi Tv tayari inapatikana katika king’ Cha Azam na sasa unaweza kuipata kupitia king’amuzi cha Startimes.

Hizi ni baadhi ya picha za matukio yaliyojiri ukumbini hapo:

 

 

Huddah Afungukia Mahusiano Yake na WCB

Socialite maarufu kutoka Kenya mrembo Huddah Monroe maarufu kama Huddah The Bosschick amefungukia uhusiano wake na Label maarufu nchini WCB.

Huddah alitua nchini Tanzania mwishoni mwa wiki hii na mara moja alionekana akiwa katika ofisi za WCB na CEO wake staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi The Playlist ya Times FM, Huddah amesema kuwa ukiachilia mbali sababu za kibiashara, amekuwa akivutiwa na uchapakazi wa timu nzima ya WCB.

The vibe is, WCB napenda sana ni watu wanajima, watu wana njaa ya maisha , so for me WCB have the some kind of vibe the i have. Wanapenda maisha mazuri, so they very work hard hawalalai saa 24 wapo kwenye kazi, so that I like that”.

Huddah ambaye ni Mfanyabiashara anayemiliki make up line yake inayoitwa Huddah Cosmetics ambayo imekuwa ikifanya vizuri.

Huddah Monroe alikuja nchini Tanzania kwa ajiili ya ku-host show ya Harmonize iliyofanyika siku ya leo June 16, 2018.

Zari Awaonya Wasafi Tv Kuwa “ Endapo Mtaendekeza Kiki za Kijinga Mtapotea”.

Mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz Zarinah Hassan ‘Zari’ amekitolea uvivu kituo cha Wasafi Tv.

Bila kujaribu kuwa mmiliki wa kituo hicho cha habari ni Diamond, Zari amewajia juu akiwataka kuripoti Habari za maana kuhusu mambo yanayoendelea nchini.

Zari alitoa povu hilo baada ya Wasafi Tv kuposti clip ya kipindi cha Refresh kinachorushwa na kituo hiko kikionyesha mahojiano waliyofanya na video Queen maarufu Irene Au Lynn.

Kwenye mahojiano hayo Irene aliulizwa endapo anamfahamu Zari ambapo alijibu kuwa hamjui Zari wa hajawahi kumsikia ambapo alisikika akisema ‘Zari Who?’.

Baada ya clip hiyo kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii Zari alienda kwenye ukurasa wa kituo hicho na kuwataka waripoti mambo ya maaan yanayoendelea Kwenye jamii badala ya kukazania mambo ya kijinga.

 

Gigy Money Adai Eti Diamond ni Baba Wa Mtoto Wake

Msanii wa Bongo Gift Stanford maarufu kama Gigy Money amerudi tena Kwenye headlines huku safari hii akidai Baba wa mtoto wake MK staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Gugy Money alijifungua mwezi uliopita lakini tangu ajifungue aliweka wazi kuwa hamjui baba wa mtoto wake kwani kipindi anapata mimba alikuwa Anatembea na wanaume wawili ambao alisema ni Mo J na Stan.

Lakini sahivi Gigy ameibuka na jipya akidai Baba wa mtoto wake pia anaweza kuwa Diamond Platnumz ambaye siku za nyuma zilishawahi kusikika tetesi kuwa aliwahi kuchepuka naye.

Gigy Money amefunguka hayo Kwenye mahojiano na Dizzim Online ambapo aliulizwa nani ni Baba wa mtoto na alifunguka:

Mo J sio Baba wa mtoto nilishasema Baba wa mtoto anaitwa Naseeb Juma Abdul au Diamond ambaye nanona bora yeye awe Baba kwa sababu ni Mlezi wa wana alafu na mimi mwenyewe Mlezi wa wana alafu kingine anapenda watoto alafu alishanichanaga Gigy ukizaa we niambie tu kwa wiki shilingi ngapi”.

Gugy Money amekuwa sana Kwenye headlines tangu ajifungue kwani ni wikiendi iliyopita inasemekana alipeana kichapo cha mwizi na mrembo Irene club.

TID- Kuna Watu Wanataka Kumshusha Diamond

Mkongwe kwenye muziki wa Bongo fleva Khalid Mohamed maarufu kama TID amefunguka na kuwatolea povu baadhi ya media ambazo zinadai a kumshusha staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

TID amedai kuwa kwa muda mrefu kumekuwa kuna utaratibu wa wadau wa muziki wa Bongo fleva kujaribu au hata kumshusha kabisa msanii pale anapothubutu kudai maslahi yake jambo ambalo amedai linaua muziki.

Kwenye mahojiano na Wasafi Tv, TID amejilinganisha na Diamond na kudai hata yeye ilishawahi kumtokea Kwenye muziki wake ambapo kuna baadhi ya vyombo vya habari vilijaribu kumshusha.

Na kweli anaweza because he has a media, yaani yeye ndio kama Mungu anajiona but mimi hapana. Nilifanya kosa hilo lakini kosa hilo ndilo limewasanua wasanii wengine, unaona msanii kama Diamond naye amekataa.

So Diamond was me lakini wakasema wewe siunajifanya mjanja sasa tunamleta Diamond tukushushe wewe. At the end Diamond naye wanataka kumuua, sijui wanataka kumuweka nani,” TID ameiambia Wasafi TV“.

Diamond ni moja kati ya wasanii ambao wamekuwa Kwenye migogoro na baadhi ya vyombo vya habari kama Clouds Fm na East Africa Tv ambavyo havipigi kabisa nyimbo zake.

“Hamisa Hata Akitaka Kuzaa Watoto Kumi na Diamond Azae Tu”-Zari

Mfanyabiashara maarufu na mama watoto wa Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zarinah Hassan amemwaga povu na kusema Hamisa hata akitaka kumzalia watoto kumi Diamond yeye kwake ruksa.

Kauli hiyo ili Jina siku ya jana baada ya Zari kuweka posti yake aliyokuwa anasherehekea kufikisha followers milioni 4 Kwenye mtandao wa Instagram ambapo shabiki alimtahadharisha kuwa kuna tetesi Hamisa ana ujauzito mwingine.

Shabiki huyo aliandika maneno haya:

Zari kuwa makini kuna tetesi huku mtaani kwetu kuwa Hamisa kashanasa mimba nyingine ila lisemwalo lipo kama halipo laja”.

Baada ya kupewa maneno hayo Zari alimjibu hata wangezaa watoto kumi yeye hana habari kwani hayumo.

Zari alijibu kwa kuandika:

Azae hata kumi mimi simo!”.

Huu ni muendelezo tu wa drama iliyoanza mwaka jana baada ya Hamisa kuanika ana ujauzito wa Diamond kwa wakati huo alikuwa mpenzi wa Zari.

Kumekuwa na tetesi tu kuwa Diamond amerudisha majeshi kwa mama watoto wake Zari baada ya kutoonana kwa muda wa Miezi minne.