Babu Tale Adai Hata Akichepuka Mke Wake Hawezi Kumuacha

Meneja wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Hamis Tale Tale maarufu kama Babu Tale amefunguka na kudai kuwa anajua hata akichepuka mke wake hawezi kumuacha.

Wikiendi iliyopita Babu Tale alisafiri kwenda nchini South Africa kwa ajili ya kuwapatanisha Diamond na mzazi Wenzake Zari baada ya kutokiwa Kwenye maelewano kwa miezi kadhaa.

Lakini tangu akiwa S.A kumekuwa na  taarifa Mtandaoni zinazodai kuwa Babu Tale amezaa mtoto na mwanamke mwingine na kumtelekeza mtoto huyo bila matunzo yoyote.

Baada ya taarifa hizo watu walimjia juu Babu Tale kwa kukimbilia kurekebisha maisha ya Diamond ilihali ya ndoa yake na mkewe  yanamshinda.

Basi Babu Tale kawamwagia povu wale wote wanaoeneza taarifa na kusema yeye na mke wake wametoka mbali wako pamoja kwa zaidi ya miaka 17 hivyo mke wake hawezi kumuacha hata afanye kosa gani.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Babu Tale alimwaga povu hili:

 

Yusuph Mlela- Diamond Anatakiwa Awapige Chini Wote Zari, Wema na Mobetto

Muigizaji za wa filamu za kibongo, Yusuph Mlela ameibuka na kumshauri Diamond awapige chini wanawake wote walio Kwenye maisha yake kwa sasa akimaaanisha Zari, Hamisa na Wema.

Mlela amefunguka hayo Kwenye mahojiano aliyefanya na Global Publishers alipoenda Kwenye sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya Gabo siku ya jana.

 

Mlela alifunguka hayo alipoulizwa  anamshauri nini Diamond kuhusu maisha yake ya kimapenzi yanayoendelea kuchoreka Kwenye mitandao ya kijamii ambapo Mlela alisema angekuwa yeye Angewapiga chini wasichana wote.

Kiukweli mimi siwezi kumshauri kitu, Diamond ana maisha yake na maamuzi yake pia, kwa hiyo yeye afurahie tu maisha yake its ok, mimi siwezi kumpangia. Ningekuwa mimi nisingekuwa nao wote (Zari, Mobeto wala Wema), siyo kwamba siwapendi, kwanza sitembei na watu maarufu ninatoka na watu wa kawaida tu”.

Diamond amekuwa akitengeneza sana headlines kutokana na Mahusiano na wanawake tofauti tofauti ambapo hivi sasa amekuwa akisemekana Kurudisha majeshi kwa Zari wakati yupo na Mobetto.

Msanii Awachana Wanawake Wanaojigonga Kwa Diamond

Msanii wa Bongo movie anayejulikana kama Mary Mawigi amewapa makavu live wanawake wote ambao wamekuwa wakijigonga kwa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Mawigi amewatolea povu hilo wanawake hao na kudai Diamond anawachezea na kuishia kuwatumia tu hao wanawake na mwishowe kuonekana kama chombo cha starehe.

Kwenye mahojiano na gazeti Amani, Mawigi alisema kuwa, wanawake ambao wako kwenye uhusiano na Diamond au wanaotamani kuwa naye wanatakiwa kujifunza kuwa mwanaume huyo amekuwa akiwachukulia kama chombo cha starehe na akichoka anachukua mwingine hivyo wasiendelee kumkubali.

Kwani Diamond ana nini cha dhahabu ambacho wanaume wengine hawana hadi wanawake wamgombee kiasi hicho?

Ninawashauri wanawake wenzangu waache kugombea au kulumbana mambo ambayo hayana faida maishani mwao, wasimame, wafanye kazi wao kama wao, maisha yataenda vizuri tu”.

Diamond ambao anajulikana kama sukari ya warembo amekuwa akidaiwa kuwa Kwenye Mahusiano ya kimapenzi na wanawake kadhaa na hata kutamaniwa na wengine wengi.

Nay wa Mitego: Babu Tale Kaiba Wazo Langu La Kuwapatanisha Diamond na Zari

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Nay Wa Mitego amemjia juu Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale huku akidai yeye ndio aliyetoa wazo la kuwapatanisha Diamond na Zari.

Mwanzoni mwa wiki hii Babu Tale alifunga Safari kwenda nchini South Africa kwa ajili ya kuwapatanisha Diamond na Zari kitendo ambao Nay amekiri kuwa ni kizuri lakini amehoji kwa nini amesubiri mpaka yeye atoe wazo hilo alafu ndio na yeye aende.

Babu Tale Alipoenda South Africa kumuombea Diamond msamaha

Kwenye na mahojiano na Risas Mchanganyiko, Nay wa Mitego amemtolea povu hilo Babu Tale:

Suala la Babu Tale kwenda kumuombea msamaha Diamond ni zuri lakini alitakiwa afanye hivyo muda mrefu na siyo asubiri mpaka nizungumze mimi kwamba nitawapatanisha. “Nashukuru wazo langu limekubalika na kila mtu na yeye mwenyewe kuliona linafaa na kufanyia kazi.

Diamond ni mshikaji wangu wa muda mrefu sana, japo mapenzi hayaingiliwi lakini kwa upande wangu namkubali sana mama Tee (Zari) maana akiwa naye mambo yake yanakuwa kwenye mstari kwani anakuwa mtu wa kazi sana tofauti na akiwa na hawa wanawake wengine.

Kutokana na kuliona hilo ndiyo maana niliona nimpe ushauri kupitia ukurasa wangu wa Instagram na kuahidi kuwarudisha pamoja, lakini kabla sijafanya hivyo, Babu Tale akalifanyia kazi, siyo vibaya nimefurahi sana kwa kweli”.

Siku video ya wimbo wa Iyena ulipotoka Nay alimshauri Diamond aachane na Hamisa na arudiane na Zari na hata kumuhaidi atasaidia kumuombea msamaha na kuwapatanisha.

Nay wa Mitego: Babu Tale Kaiba Wazo Langu La Kuwapatanisha Diamond na Zari

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Nay Wa Mitego amemjia juu Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale huku akidai yeye ndio aliyetoa wazo la kuwapatanisha Diamond na Zari.

Mwanzoni mwa wiki hii Babu Tale alifunga Safari kwenda nchini South Africa kwa ajili ya kuwapatanisha Diamond na Zari kitendo ambao Nay amekiri kuwa ni kizuri lakini amehoji kwa nini amesubiri mpaka yeye atoe wazo hilo alafu ndio na yeye aende.

Babu Tale Alipoenda South Africa kumuombea Diamond msamaha

Kwenye na mahojiano na Risas Mchanganyiko, Nay wa Mitego amemtolea povu hilo Babu Tale:

Suala la Babu Tale kwenda kumuombea msamaha Diamond ni zuri lakini alitakiwa afanye hivyo muda mrefu na siyo asubiri mpaka nizungumze mimi kwamba nitawapatanisha. “Nashukuru wazo langu limekubalika na kila mtu na yeye mwenyewe kuliona linafaa na kufanyia kazi.

Diamond ni mshikaji wangu wa muda mrefu sana, japo mapenzi hayaingiliwi lakini kwa upande wangu namkubali sana mama Tee (Zari) maana akiwa naye mambo yake yanakuwa kwenye mstari kwani anakuwa mtu wa kazi sana tofauti na akiwa na hawa wanawake wengine.

Kutokana na kuliona hilo ndiyo maana niliona nimpe ushauri kupitia ukurasa wangu wa Instagram na kuahidi kuwarudisha pamoja, lakini kabla sijafanya hivyo, Babu Tale akalifanyia kazi, siyo vibaya nimefurahi sana kwa kweli”.

Siku video ya wimbo wa Iyena ulipotoka Nay alimshauri Diamond aachane na Hamisa na arudiane na Zari na hata kumuhaidi atasaidia kumuombea msamaha na kuwapatanisha.

Mr. Blue- Sina Tatizo na Diamond Ila Kuna Watu Wanataka Tuwe na Bifu

Msanii mkongwe wa Bongo fleva Khery Sameer  maarufu kama Mr. Blue amefunguka na kudai binafsi hana tatizo lolote na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz bali kuna watu wanataka wawatengenezeee bifu.

Kwa muda mrefu imekuwa ikisemekana kuwa Diamond na Mr Blue wana bifu kutokana na mara kadhaa Mr Blur amesikika akimtupia madongo mazito Msanii huyo.

Lakini juzi Mr. Blue amethibitisha kuwa hana tatizo lolote na Diamond na hata akauposti Wimbo Mpya wa Diamond #Iyena na kuupa promo.

Lakini pia Kwenye Interview aliyofanya na Wasafi Tv, Mr. Blue amefunguka na kuweka wazi kuwa hana tatizo na Diamond kwani alianza kumsapoti tangu akiwa underground:

Ukikaa na Diamond ukamuuliza atakwambia kuwa mimi nimeanza kumpa sapoti tangu mwanzoni Wakati Diamond hajulikani na waandishi wa habari, hajulikani na mtu yoyote.

Hapo inaonyesha wazi kuwa sina chuki na Diamond wala sina tofauti naye yoyote kama ningekuwa na chuki ningemzuia tangu anaanza kutoka hata nyie msingekuwa na kazi”.

Lakini pia Mr Blue aliendelea kufunguka:

Kinachonichekesha kunishangaza ni pale watu wanapooana nimemsapoti akiwa na mafanikio wanataka nianze kumkandia kitu ambacho hakiwezekani. Mimi Diamond ni mdogo wangu wakati anatoka sikuwahi kuwa na bifu naye wala tofauti naye, kuna I wanaotaka kutuingiza katika tatizo mimi na Diamond”.

 

 

ShiiKANE- Diamond ni Msanii Anayejituma Hata Kama Humpendi, Utakubali Kazi Zake

Kundi la muziki kutoka Nigeria linaloundwa na wadada watatu wanaojulikana kama ShiiKANE wamefunguka na kumkingia kifua staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Miezi michache iliyopita Diamond alishinda tuzo ya msanii bora wa kuime nchini Nigeria na kuwabwaga mastaa wakubwa kama Davido kitendo ambacho kiliwakera Wanigeria ambao waliweka wazi kuwa hawakupenda Diamond kushinda.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Kundi hilo la ShiiKANE kutoka Nigeria linasema Diamond alistahili tuzo hiyo kutokana na ukweli usiopingika kuwa ni mchapakazi na kazi zake ni nzuri.

Ni mtu anayejituma hata kama haupendi au kupenda muziki wake lazima ukubaliane na anachikifanya kwa sababu anastahili kushinda alichokishinda. Kila utakapomuongea basi jua ndivyo anavyozidi kuwa juu”.

Katika tuzo hizo Diamond alishinda katika kipengele cha Best Male MVP na kuwabwaga wasanii kama Runtown, Davido, Olamide, 2face Idibia, Wizkid, Shatta Wale, Navio na Sarkodie.

Ommy Dimpoz Afunguka Kuhusu Bifu Lake na Diamond

Staa wa muziki anayefanya vizuri kwa hivi sasa na kibao chake cha ‘Yanje’ Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz amefunguka kuhusu bifu lake na msanii mwenzake Diamond Platnumz.

Ommy Dimpoz na Diamond walikuwa marafiki kwa muda mrefu na hata kutoa pamoja nyimbo kali kama Prokoto na nyinginezo.

Lakini wasanii hao waliingia katika bifu zito miaka michache iliyopita hadi kupelekea wawili hao kupelekana polisi baada ya Ommy Dimpoz kumuongelea mama Diamond Mtandaoni.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Citizen Radio hivi karibuni Kwenye Media your nchini Kenya Ommy Dimpoz alipoulizwa kama bifu lake na Diamond litaishia alifunguka:

Kila jambo lina wakati wake kwa hiyo time itakapofika mambo yote yatakaa sawa, tuombe Mungu”.

Lakini pia Kutokana na mgawanyiko uliopo kati ya WCB na Team Kiba, Ommy Dimpoz aliulizwa endapo kuna nyimbo zozote anazozipenda kutoka kwa WCB:

Moja wapo ni hiyo kama unavyosema Kwa Ngwaru ni wimbo ambao unafanya vizuri, yeah!, kuna mwingine nimesikia wa Rayvanny Pochi Nene, kwa hiyo kwa currently ni nyimbo ambazo naweza kusema zinafanya vizuri“.

 

Mama Diamond- Sitakubali Diamond Apotezwe na Mwanamke

Mama Mzazi wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Bi Sandra maarufu kama Mama Diamond ameweka wazi kuwa hataruhusu mwanaye apotezwe na wanawake wanabe.

Kauli hiyo ya Mama Diamond imekuja baada ya maneno maneno mengi kuzuka baada ya yeye kushangilia Diamond kurudiana na Zari huku akijua wazi kuwa yupo na Hamisa.

Mama Diamond ameweka wazi kuwa hamtaki Hamisa kama mkwe wake kauli iliyosababisha mashabiki kumjia juu kwa kitendo chake cha kutaka kumchagulia mtoto wake mke.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mama Diamond amesema wazi kuwa hawezi kukubali kuona Diamond anapotea na yeye kama mzazi yupo kwa ajili ya kumuweka katika njia iliyonyooka:

Diamond- Mwanamke Mvuto wa Sura Kwanza Tabia Baadae

Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amefunguka na kudai kuwa akiwa anatafuta mwanamke anaangali sura kwanza mambo ya Tabia yanafuata baadae.

Diamond ameweka wazi kuwa kigezo chake kikubwa anachotumia katika kusaka mwanamke wa kuoa kwanza ni sura na sio Tabia kama wengi wanavyodai.

Kwenye mahojiano yake na kipindi cha Kaa Hapa cha TBC 1, Diamond ameweka wazi kuwa yeye anaangalia sura zaidi kwa sababu sura huwezi kuibadilisha lakini tabia unaweza ukmbadilisha mwanamke.

Kiukweli tabia tunapenda lakini wakati mwingine sura nazo zina uzito wake, Kiukweli tabia mnaweza kuelekezana ila sura kuelekezwa mtaelekezana vipi?. Tabia tunajifunza kama alijifunza kuchukia atajifunza kupenda, sura atajifunza vipi?, Kwa mwanamke mimi naangalia sura kwanza , tabia tutaelekezana”.

Lakini pia Diamond amesema kuwa kama angetoa asilimia kwa vigezo vya sura na tabia basi asilimia 70 angetoa kwa upande wa sura na asilimia 30 zilizobaki ndio angeangalia tabia.

Abdu Kiba- Ninaweza Kufanya Kolabo na WCB Lakini Inategemea na Wimbo

Msanii wa Bongo fleva Abdul Kiba ambaye pia ni mdogo wa staa wa Bongo fleva Ali Kiba amefunguka na kudai kuwa yupo tayari kufanya Kolabo na mahsimu wao wakubwa WCB.

Sio siri kuwa Diamond na Ali Kiba hawapikiki chungu kimoja pamoja na kwamba wameshasema hawana bifu lolote lakini ni wazi kuwa Kumekuwa na tensions fulani baina ya makundi hayo mawili.

Lakini Abdu Kiba ameibuka na kudai kuwa kama ikitokea kuwa kuna wimbo ambao utakuwa na uhitaji wa msaniii kutoka WCB ndio ukae sawa hataona shida kumtafuta ili wafanye kazi.

Abdu Kiba amefunguka hayo Kwenye mahojiano na EFM Radio Lakini amejitetea Kuwa Mpaka sasa hajapata wimbo unaohitaji sauti kutoka kwa msanii yeyote wa WCB:

Kufanya kolabo na msanii yeyote kutoka WCB inategemeana na muziki gani ambao nimeimba, naamini kila muziki una sura ambayo inaonyesha ni nani unaweza kuimba naye, ikitokea kuna muziki ambao naona kuna haja ya msanii kutoka WCB nitafanya naye na kama sina tutabaki hivi hivi WCB na Team Kiba”.

 

Nay wa Mitego Amshauri Diamond Amuoe Zari Aachane na Hamisa

Staa wa muziki wa Bongo fleva Nay wa Mitego amemtaka Msanii mwenzake Diamond Platnumz amtupie kule mpenzi wake wa sasa na arudishe majeshi kwa Mama watoto wake Zari.

Suala hili lilikuja siku chache zilizopita baada ya Diamond kuachia wimbo wake mpya unaoitwa Iyena ambao ndani yake video queen ni Ex wake Zari.

Nay wa Mitego ambaye alishawahi kuweka wazi tangu Diamond alipoachana na Zari kuwa yeye anampenda Zari awe na Diamond.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nay wa Mitego aliandika ujumbe huu kuhusu wimbo huo na ZAri:

Mzee Mwenzangu Diamond platnumz Hii Ngoma Iyena Ata Ungeenda Kuacha Tu Barabarani Ukajifanya Kama Umeitupa Inge Hit Tu. Licha Ya Kwamba Ngoma Kali Pia Upo Na Mkeo Original Mama Tee Mwenye Nyota Ya Hela Na Mafanikio. Sasa Wewe Endelea Kupuyanga Na Hao Mapugi Machafua Nyota. Nitaongea Na Mama Tee Yaishe Tu.(Yamoyoni) Haya Fanya Muende YouTube”.

Nay wa Mitego na Diamond walitoa hit iliyokwenda jina la Muziki gani, hata hivyo hawakuishia hapo baadaye walitoa ngoma nyingine inaitwa ‘Mapenzi Pesa’.

Hamisa Mobetto Ndani Ya Bifu Zito na Familia Ya Diamond

Mzazi mwenza na mpenzi wa Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Hamisa Mobetto amejikuta katika kiti cha moto baada ya familia ya Diamond kumgeuka na kumuwashia moto kwenye mitandao ya kijamii.

Sakata hili lilianza siku ya Ijumaa baada ya  Diamond kuachia wimbo na video yake mpya ya wimbo unaoitwa Iyena aliomshirikisha Rayvanny ambapo ndani ya wimbo huo Video Queen ni Zari.

Sio siri kuwa Hamisa pamoja na kwamba amerudiana na Diamond lakini hana uhusiano mzuri na familia ya Diamond ambayo ilishaweka wazi kuwa hainpendi na haimaanishi kwani ni juzi tu kulikuwa na sakata kati ya Hamisa na Mama Diamond.

Baada ya wimbo huo wa Iyena kutoka mara moja ya Mama Diamond alianza kuposti wimbo huo na vijembe juu kwa hamisa na kudai kuwa ni mchafu hajui hata kutandika kitanda huku akimsifia Zari na alionyesha wazi kuwa anataka mwanaye arudiane na Zari.

Hata Dada wa Diamond, Esma alimtolea povu Hamisa na kuweka wazi kabisa kuwa amemiss Zari na kuandika ujumbe huu:

Familia ya Diamond ilionyesha wazi kuwa hamtaki Hamisa huku ikidaiwa chanzo cha kumchukia ni baada ya Hamisa kuwaitia Shilawadu siku walioenda hospitali kumuangalia alipokuwa amejifungua.

ShiiKANE- Tunatamani Kufanya Kazi na Diamond Lakini Ali Kiba Kwanza

Mastaa wa muziki kutoka Nigeria ShiiKANE wamefunguka na kuweka wazi kuwa wanatamani sana kufanya kazi na Diamond lakini mpaka wakishafanya kazi na Ali Kiba Kwanza.

Wasanii hao watatu wanaounda kundi hilo la ShiiKANE wapo nchini Tanzania kutoka nchini Nigeria kwa ajili ya kufanya kazi na baadhi ya wasanii wa nchini hapa Lakini pia kwa ajili ya kutangaza muziki wao.

Wasanii hao wamekiri kuwa wanatamani kufanya kazi na wasanii wa Bongo Diamond na Ali Kiba lakini mmoja wa wadada wa kundi hilo Shay amekiri kuwa wanataka kufanya kazi na Ali Kiba kwanza.

Wasanii hao walifunguka hayo Kwenye mahojiano waliofanya na Bongo 5:

Tunatamani kufanya kazi na mtu kama Diamond ila kwanza Alikiba kisha Diamond ila tayari tumesha fanya kazi na Chin Bees ambaye ametufundisha Kiswahili kidogo katika kazi tuliyofanya“.

Lakini pia mbali na Diamond na Ali Kiba ShiiKANE wamesema Msanii wanaye ramani kufanya naye kazi ni Vanessa Mdee kwani wamekiri wanavutiwa na kazi zake sauti  yake na hata urembo wake.

Mchungaji Lusekelo Awashauri Diamond na Ali Kiba Waache Uzinzi

Mchungaji wa kanisa la Maombezi (GRC) mchungaji maarufu anayejulikana kama Mzee wa Upako amewataka wasanii Diamond Platnumz na Ali Kiba waache uzinzi.

Siku chache zilizopita Mchungaji Lusekelo alitengeneza headlines baada ya kusema kuwa anamkubali sana Diamond kwa sababu ni mnyenyekevu na akamkosoa Ali Kiba kuwa ni mjeuri.

Kwenye Interview yake na Millard Ayo Tv, Mchungaji Lusekelo amesema hawezi akakaa na kujibizana na Diamond wala Ali Kiba kwa sababu wote ni watoto sana kwake anaweza kuwazaa.

Lakini pia Mchungaji Lusekelo amewapa ushauri wasanii hao na kuwataka  waache uzinzi kwani maisha ni mafupi:

Muache uzinzi haya maisha ni mafupi sio leo una mke huyu kesho una mke yule mtakufa!.

Mimi ni Mzee ingawa sio Mzee sana lakini nimeishi maisha marefy lakini tumeona wanamuziki wengi walikuwa lile juu wanakuja wanaporomoka na mwenye akili hujifunza Kupitia makosa ya watu wengine lakini mjinga hujifunza kwa makosa yake mwenyewe”.

Lakini pia Mchungaji Lusekelo aliwataja wasanii wengine ambao anawakubali mbali na Diamond ambao ni Ben Pol, Darassa, Mrisho Mpoto na Malaika.

Shetta Ataja Sababu Ya Kutofautiana na Diamond

Staa wa muziki wa Bongo fleva Shetta amefunguka na kuweka wazi sababu hasa za yeye kutofautiana na msanii mwenzake Diamond Platnumz.

Shetta na Diamond mbali na kufanya kazi wote na kutengeneza hits mbali mbali Lakini pia walikuwa ni marafiki wa karibu lakini siku za hivi karibuni wamekuwa hawaonekani pamoja.

Kwenye mahojiano na Wasafi Tv, Shetta amefunguka na kusema hakuna bifu kati yake na Diamond kama watu wengi wanavyodhani bali wametangana kwa sababu za kibiashara:

Sidhani kama kuna bifu lakini mimi nafikiri biashara sababu mwanzo tulikuwa tunaishi kama washikaji lakini ikimbukwe sote ni wanamuziki ili kutafuta inabidi kila mtu apambane.

Siri ya biashara kila mmoja anataka kufanikiwa, kila mmoja anataka kuwa namba moja na kuna series za mafanikio. Automatic wewe kama mwanamuziki na sifaidiki na wewe kwa njia moja au nyingine, siwezi kukupa njia zangu na wewe huwezi kunipa njia zako lakini haiwezi kuwa kama tatizo”.

Wasanii hao wameshafanya ngoma kali kama vile Nifanganye na kerewa.