Harmonize Afungukia Ushindani Uliopo WCB

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka WCB Harmonize amefunguka na kuelezea ugumu uliopo katika kufanya kazi kama msanii wa label ya WCB kutokana na ushindani.

Harmonize amefunguka na kuweka wazi kuwa ushindani ndani ya Label hiyo kati ya wasanii ambao wapo ndani ya Label ndio ugumu ambao upo humo.

Kwenye mahojiano na Planet Fm, Harmonize amesema ugumu uliopo WCB ni kila msanii ana uwezo mkubwa, hivyo kila mmoja anahakikisha anafanya kazi nzuri.

Ugumu ni pale ambapo unafanya kazi na wasanii wote ambao ni talented, so way competion katika kurekodi ngoma kila mtu anataka kutoa ngoma yake kali kumshinda mwenzake, so ugumu unaanzia hapo“.

WCB ni Label kubwa kabisa Tanzania na inabeba wasanii wanaofanya vizuri sana, wasanii hao kama vile Diamond Platnumz, Rayvanny, Harmonize, Rich Mavoko, Mbosso na wengineo.

 

Harmonize Atangaza Ujio Wa Albamu Yake

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB, Harmonize ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Kwangaru’ ametangaza ujio wa albamu.

Harmonize ametangaza Habari hiyo njema kwa mashabiki zake wanaopenda muziki wake kwani hiyo ndio itakuwa albamu yake ya kwanza tangu aanze kufanya Muziki.

Kwenye Interview yake na Bongo5, Harmonize amefunguka kuwa analazimika kutoa albamu kwa sababu ndio utambulisho rasmi wa msaniii ndani ya tasnia ya muziki.

Nipo ndio nashughulikia albamu yangu lakini nipo kwenye hatua za mwisho sana, so muda wowote naweza kuitangaza lini itatoka, itakuwa na wasanii tofauti tofauti“.

Siku za nyuma Diamond Platnumz alishawahi kufunguka kuwa wasanii wote wa WCB wanatoa Albamu zao kwa muda fulani ambapo yeye ameshatoa albamu yake ya ‘A boy from Tandale’.

 

Harmonize Athibitisha Kuwa “Singe Boy’

Baada ya kuwa na mikwaruzano na kufikia mwanadada Sarah ambae ndie mpenzi wake na harmonize kuandika katika mitandao ya kijamii huku akitukana kumlenga mwanaume wake Harmonize kuwa amekuwa akimsaliti, mwanamuziki huyo ameweka picha katika ukurasa wake wa instagram akisema kuwa  yeye sasa hivi ni single boy akimaanisha kuwa hana hayuko tena katika mahusiano ya kimapenzi.

Maneno ya Sarah kuhusu kuchepuka na Harmonize yanakuja baada ya mwanamuziki huyo kuwepo nchini Nigeria ambapo inasemekana kuwa alikuwa akitoka kimapenzi na moja ya watangazaji nchini humo aliyejulikana kwa jina la Nancy.

 

Harmonize Asema Hana Bifu na Mwarabu Fighter

Kulikuwa natuhuma za kuwa mwanamuziki harmonize hana mahusiano mazuri na body guard wao kwa sababu ya tetesi zilizowahi kusambaa kuwa alikuwa katika mahusiano ya kimapenzi na sarah ambae ni mpenzi wa harmonize.

Akiongea na waandishi wa habari siku ya jana , Harmonize alifunguka na kusema kuwa  Yeye na mwarabu fighter hawana mahusiano mabaya wala ugomvi wowote  na hata maneno mabaya aliyowahi kuzushiwa yalikuwa hayana ukweli wowote.

katika mahojiano yaliyowahi kupita huku nyuma, sarah, mwarabu fighter na hata harmonize mwenyewe aliwahi kukanusha taarifa hzio na kusema kuwa maneno hayo hayana ukweli  wowote.

Harmonize Amkingia Kifua Mobetto Baada Ya Kugeukwa na Kila Mtu

Staa wa muziki wa Bongo fleva Harmonize ameonekana kuwa upande wa Hamisa Mobetto na kumkingia kifua baada ya kila mtu kumtolea povu.

Sakata hili lilianza siku ya Ijumaa baada ya  Diamond kuachia wimbo na video yake mpya ya wimbo unaoitwa Iyena aliomshirikisha Rayvanny ambapo ndani ya wimbo huo Video Queen ni Zari.

Baada ya video hiyo kutoka karibia kila mtu kuanzia familia ya Diamond mpaka WCB wote walianza kumposti Zari huku wakimtaka arudi kwa Diamond na kumponda kabisa Hamisa.
Harmonize pekee alionekana kuwa upande wa Hamisa kwani baada ya kila mtu kwenda upande wa Zari Harmonize alimpa moyo Hamisa ambapo aliandika ujumbe huu:

Lakini pia hata Kwenye mahojiano aliyofanya na WAsafi Tv Harmonize alipoulizwa kwanini peke yake ameamua kuwa uapnde wa Hamisa alijibu kuwa yeye ni kama bendera fuata upepo kwani Diamond alisema yupo na Hamisa basi atakuwa upande huo na alisema kwa MObetto na yeye atakuwepo huko.

Diamond Akiri Kumkubali Mrisho Mpoto Kwa Staili Yake Mpya

Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz amemvulia kofia  na kuonyesha kumkubali Msanii Mrisho Mpoto baada Ya staili yake aliyotumia kuimba wimbo alioshirikishwa na Harmonize unaoitwa Nimwage Radhi

Msanii Mrisho Mpoto ameshazoeleka kwa staili yake moja ya uimbaji aliyoitumia Kwenye nyimbo zake maarufu kama Mjomba, Zisonje na Njoo Uzichukue na nyinginezo.

Lakini Kwenye Wimbo Mpya alioshirikishwa na Harmonize ambao sasahivi unafanya vizuri sana Nimwage Radhi Mpoto amekuja kwa staili nyingine kabisa ya kuimba na kuwafurahisha watu wengi ikiwemo Diamond Platnumz.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond ameshindwa kujizuia na kumwagia sifa Mrisho Mpoto ambapo ameandika:

Kwa kweli Mrisho Mpoto nilikuwa nakuwaza sana, Kwa ufanisi wa serikali hii, ungewezaje kutupa vile vibao vyako vya #MJOMBA #WAITE Na Kadharika…. ila nimeamini kweli Mungu kakutunuku Kipaji na Ubunifu wa Sanaa, Sikutegemea kama UtaniSurprise namna hii… #NimwageRadhi Kali sana?? ….Mdogo angu Mmakonde @harmonize_tz naona Mwaka Huu unahasira nao sana….Kama Naiona hiyo #WasafiFestival Huu Mwaka Sjui hata tuanzie Mkoa gani???,” aliandika Diamond Instagram“.

Wimbo huo umekuwa ukifanya vizuri na kushika chati katika vituo mbali mbali vya habari na hata kushika nafasi za juu katika mtandao wa Youtube.

Shamsa Ford: Sina Bifu na Harmonize

Muigizaji wa Bongo movie Shamsa Ford amefunguka na kusema hana bifu lolote na staa wa muziki wa Bongo fleva Harmonize hata baada ya kumdhalilisha mume wake .

Wiki chache zilizopita Harmonize alikuwa kwenye vita kali ya Ex wake Jacqueline Wolper na katika ugomvi wao alimtaja mume wa Shamsa Chidi Mapenzi kama mmoja wa mpenzi wa zamani wa staa jambo ambalo lilimkera Shamsa.

Shamsa aliweka wazi kuwa hajafurahishwa na maneno ya Harmonize kumuingiza mume wake Kwenye bifu lake na Wolper na kumdhalilisha wakati anajua wazi kuwa ameoa tayari.

Kwenye mahojiano na FNL ya EATV, Shamsa amesema kuwa licha kutopendezwa na kitendo hicho kwa ujumla hana ugomvi na Harmonize ili maisha mengine yaendelee.

Mume wangu ni mtu mpole sana, inawezekana hakupendezwa ila alikaa kimya, sisi wanawake tunamunkari ya hali ya juu, halafu unaona huyo kapata wapi huo ujasiri wa kuweka hivyo bila kufikiria hawa watu wengine tayari wana familia zao.

Nilipaniki lakini mwisho wa siku simchukii na sina bifu naye niliongea nilichokuwa najisikia na yameisha na hata tukikutana tunasalimiana vizuri kwa sababu hatuna bifu. Sisi ni vijana tunahitaji kuweka nguvu nyingi sana katika kufanya kazi na sio mabifu”.

 

Harmonize Atoboa Siri ya Video ya Dai na Hamisa Kuvuja

Msanii harmonize amefunguka na kusema kuwa video ndogo iliwahi kuvuja katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha Daimond na Hamisa kuwa wako fargaha akiwa na wanwake wawili tofauti ni sehemu ndogo ya movie inayokuja wakiwa location.

Harmonize amefunguka hayo akiwa katika kituo cha Citizen na kusema kuwa  movie hiyo yenye lngo la kutoa elimu kwa jamii kuhusu unyanyasaji wa wanawake  katika ndoa na mahusiano.

Walikuwa wakishuti mobie nayoelezea jinsi wanaume wamekuwa wakidhalisha wanwake katika mahusiano,sasa ili iweze kuleta attentio kwa watu na piaiwe item  of bussiness waliona ni bora kumtumia diamond ambae ameshakuwa katika mahusiano mara nyingi na watu tofauti tofauti.

Video hiyo uliyosambaa sana ilizua gumzo lakini pia iliwafanya wasanii hawa kuongelewa mpaka katika bunge na kisha wasanii hawa kuwekwa chini ya ulinzi kwa ajili ya mahojiano lakini walikuonywa na kuomba msamaha kwa jamii.

Harmonize- Wanaume Waaminifu Africa Wanatoka WCB

Msanii wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB, Harmonize amefunguka na kudai kuwa wanaume waaminifu kutoka Africa Mashariki wanatoka WCB.

Kwa mara ya kwanza kauli  kama hiyo ilitolewa na mmoja kati ya mameneja wa WCB, Babu Tale mapema mwaka jana ambapo ilipingwa na watu kadhaa ikiwemo Aunty Ezekiel.

Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Kwa Ngwaru’ ameiambia Mambo Mseto, Citizen Radio kuwa kitu hicho ni cha kweli kabisa na uamifu wao umevuka mipaka, sio Bongo tu.

Ni kweli kabisa asilimia mia moja, hamna matukio halafu sisi ndio tunangoza kwa kusalitiwa“.

Kauli hii Inawaacha hoi watu wengi kwa sababu karibia wasanii wote WCB wanakabiliwa na skendo za kuchepuka kuanzia tu na CEO mwenyewe Diamond Platnumz ambaye skendo yake ya kuchepuka na Hamisa wakati yupo na Zari ilitrngeneza headlines.

Mrembo Aliyedaiwa Kubeba Ujauzito Wa Harmonize Aomba Radhi

Mrembo ambaye ni msanii wa nyimbo za Injili kutoka Kenya anayejulikana kama Veronica Wanja ‘Nicah The Queen’ amewaomba radhi mashabiki zake baada ya taarifa kuenea Kwenye mitandao ya kijamii kuwa ana ujauzito wa Harmonize.

Wiki iliyopita kuna picha iliyosambaa Kwenye media iliyomuonyesha Harmonize na Mrembo huyo wakiwa kwenye pozi zero distance hali iliyopelekea kuibua Tetesi za kuwa wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Veronica ametumia ukurasa wake wa Instagram kuwaomba radhi mashabiki zake lakini pia kanisa lake kwa stori hiyo ya kumchafua na kusisitiza kuwa yeye sio mjamzito kabisa na wala hana uhusiano na Msanii huyo.

I owe all my fans the truth and an apology for all those who support my ministry, I have never been into a relationship with Harmonize, I’m not pregnat . We took this photo sometime last year at the studio, I have never met him again ever since.

Harmonize is in a loving and serious relationship with his girlfriend. I admire his hard work and I like his music. There’s nothing between me and him”.

Baada ya Tetesi hizo Harmonize ameonekana mkoani Mwanza na mpenzi wake Sarah walipoenda kufanya shoo siku ya Jumamosi.

Engine Amkingia Kifua Wolper Dhidi Ya Harmonize

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Engine amemkingia kifua aliyekuwa mpenzi wake Jacqueline Wolper dhidi ya Ex wake Harmonize baada ya sakata lao Siku mbili hizi.

Bifu la Wolper na Harmonize lilifika pabaya kiasi ya kwamba Harmonize alianika listi nzima ya wanaume ambao Wolper amebanjuka nao kitendo kilicho wakera watu wengi.

Engine ametumia ukurasa wake wa Instagram kumuandikia Wolper barista ya wazi huku akimuahidi kuwa hataweza kumdharau au kumchafua kamwe kwani yeye ni mshindi Kwenye macho yake.

God Never rust….My prophecy…..U will always be there because your a Winner Wolper.Nakuheshimu sana liwake jua inyeshe mvua…Katika vitu sitaweza kuja kufanya ni kumdharau mwanamke awaye yoyote maana hata kama mwanaume ni kichwa basi mwanamke ni shingo na kiwiliwili usiisahau ‘A’ kisa umeijua ‘B’ maana huwezi kuandika majina makubwa ya Kiswahili kama Mama na Baba bila kutumia A”.

Engine alikuwa Kwenye Mahusiano na Wolper na hata walitangaza kufunga ndoa na juzi Harmonize amethibitisha Mahusiano yao baada ya kumuweka Kwenye listi ya wanaume wa Wolper.

Jacqueline Wolper Amvulia Kofia Harmonize

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Jacqueline Wolper amemvulia kofia aliyekuwa mpenzi wake msanii wa Bongo fleva kutoka WCB, Harmonize na kukubali bifu lao liishe.

Kwa muda wa wiki nzima sasa Wolper na Harmonize wamekuwa Kwenye vita ya maneno Kwenye mitandao ya kijamii huku kila mmoja akidai mwenzake bado anampenda na bado anamtaka.

Wolper ameamua kupiga kimya ili bifu lao lilikuwa linaendelea liishe tofauti na juzi na siku zilizopita ambapo alikuwa akipewa Dongo lolote na Harmonize alikuwa anajibu.

Siku ya jana Harmonize alihaidi kuendeleza mtanange huo baada ya kudai anataka kuweka listi nyingine ya wanaume waliotembea na Wolper baada ya mara ya mwisho kuweka listi ya wanaume kumi na mbili.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Wolper aliandika ujumbe huu kuashiria hatomjibu Tena Harmonize:

Mungu nifundishe kunyamaza, we ndio unaujua ukweli #Najifunzakuheshimkilangaziiliyonifikishanilipo
#NdiomaanataupambanesiwezkushukaatanishushaMungupekee #jifunzekuheshimkilangaziiliyokufishaulipokamweutoteterekakwajarbulolote
#MunguwanguwaushindiwewenijbuToshaNimekukabidhiwewekilakitu

 

Muimbaji Wa Injili Nchini Kenya Aliyedaiwa Kubeba Mimba Ya Harmonize Afunguka

Siku mbili hizi kuna stori zilienea Kwenye mitandao ya kijamii  zilizosema kuwa Msanii wa Bongo fleva kutoka WCB Harmonize amempachika mimba mwanadada ambaye ni msanii wa nyimbo za Injili kutoka Kenya.

Msanii huyo anayejulikana kama Veronica Wanja ‘Nicah The Queen’ amekataa tuhuma hizo na kudai kuwa hazina ukweli wowote, awali Nicah alikuwa katika mahusiano na mchekeshaji Dr. Ofweneke’s.

Tetesi hizi zimekuja mara baada ya wasanii hawa kuonekana pamoja mara kwa mara hali iliyozua minong’ono.

Kwenye Interview aliyofanya na gazeti moja nchini humo Veronica alisisitiza kuwa yeye sio mjamzito na hapendi kuongelea sana hayo mambo kwa sababu yeye ni Msanii wa injili hivyo si vema kuongelea.

 

Shamsa Ford Amjia Juu Harmonize Kwa Kuingilia Ndoa Yake

Msanii wa Bongo fleva kutoka label ya WCB Harmonize amepokea makavu live kutoka kwa mwanadada anayefanya vizuri kwenye tasnia ya Bongo movie Shamsa Ford baada ya kumuorodhesha mumewe Chidi Mapenzi Kwenye orodha ya Wolper.

Siku ya jana Wolper, Harmonize na Sarah walikuwa kwenye vita kali ya Kwenye mitandao ya kijamii na katika harakati hizo Harmonize alianika orodha nzima ya wanaume ambao Wolper amewahi kujivinjari nao na mmoja kati ya watu hao ni Chidi Mapenzi.

Chidi Mapenzi ni mume halali kabisa wa Shamsa Ford kwaiyo baada ya kusikia mumewe katajwa Kwenye orodha hiyo alishindwa kujizuia kwani alikuja juu bibaya mnoo na kumtaka Harmonize amkome mumewe na asimuingize Kwenye ugomvi wao.

Shamsa alienda kukomenti maneno haya Kwenye posti ya Harmonize:

Harmonize nakuheshimu sana mdogo wangu pls nisingependa kuona jina la mume wangu Kwenye huo ujinga wenu. Chidi kwenu anaweza akawa mshkaji kwangu mimi ni mume kulikuwa hakuna haja ya wewe kuweka jina lake wakati unajua ana maisha mengine. Tusichukuliane Poa”.

 

Harmonize Awasihi Mashabiki Wasimchonganishe na Ali Kiba

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘ Kwa ngwaru’ Harmonize ameibuka na kuwasihi mashabiki zake wasimchonganishe na msanii mwenzake Ali Kiba.

Kwa muda mrefu kumekuwa na sintofahamu kati ya Diamond na Ali Kiba hali iliyosababisha kuwepo hata kwa uadui kati ya wasanii wa WCB au watu wake wa karibu na watu wa karibu wa Ali Kiba.

Siku ya Jumapili kwenye viwanja vy Leaders Club Ali Kiba na Diamond walizua gumzo baada ya kusalimiana msibani kuonyesha kama hakuna tofauti baina yao.

Lakini Harmonize alikaaa pembeni ya Ali Kiba lakini kilichowashangaza watu wengi ni baada ya kuonekana hawajaongea neno hata moja yaani kiufupi walichuniana.

Baadae mashabiki walimjia juu Harmonize na kudai alimchunia Ali Kiba hakumpa hata salamu wakati bosi wake Diamond alijishusha na akamsalimia Ali Kiba.

Harmonize amemtolea povu shabiki kupitia mtandao wa Instagram na kumtaka asimgombanishe na Ali Kiba:

 

 

Harmonize Amefungukia Kuvunjika Kwa Mahusiano Ya Zari na Diamond

Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka label ya WCB Harmonize kwa mara ya kwanza amefungukia suala la kuvunjika kwa Mahusiano ya Zari na Diamond Platnumz.

Miezi miwili iliyopita siku ya wapendanao Zari alitumia ukursa wake wa Instagram kumwaga aliyekuwa mpenzi wake Diamond baada ya kuzidisha michepuko ingawa suala hilo lilitokea muda mrefu uliopita lakini mpaka leo linatrend.

Harmonize mbali ya kuwa msanii wa Diamond lakini pia ni mtu wa karibu ambaye pia alikuwa na ukaribu na Zari kwaiyo alipoulizwa anachukuliaje wawili hao kuachana alisema anaheshimu maamuzi ya Zari.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Funiko Base ya Radio Five, Harmonize amefunguka na kusema kuwa yeye binafsi anaheshimu maamuzi ya Zari kwa sababu ana maamuzi yake binafsi.

Mimi naheshimu sana maamuzi ya mtu siwezi kuongea kama ni vibaya au ni vizuri Kwanza muda wa kumshauri mtu kuhusu Mahusiano Yake ndio sina”.

Lakini pia Harmonize alisisitiza kuwa hawezi kumuongelea sana Zari na kuorodhesha mambo ambayo alimsaidia kwani unaweza ukaonekana mnafki.