Lava Lava awatetea wasanii wa Wasafi records baada ya wengi kudai kuwa wanamuiga Diamond Platnumz

Lava Lava ambaye ni msanii mpya wa Wasafi records kwa hivi sasa anatamba kwa wimbo wake mpya ‘bora tuachane’ ambao umempa mashabiki wengi kwa muda wa wiki moja.

Baada ya kuingia Wasafi msanii huyu amepata interview kadhaa kwa redio na hivi karibuni tunatarajia kumuona kwenye televisheni.

Lava Lava
Lava Lava

Hata hivyo kama wasanii wenzake, msanii huyu ameweza kupata changamoto ambazo zinaweza kuiletea career yake shida. Hivi karibuni akizungumza kwenye interview na Bongo 5 msanii huyu alikana kuwa hakuna msanii yoyote kutoka Wasafi Records anayemuiga Diamond Platnumz. Kulingana na yeye kila mtu ananjia tofauti ya kuimba na iwapo saa zingine wengi wanaona kuwa wanaimba kama mkubwa wao…hii sio ukweli.

Alisema,

“Naona watu wanazungumza lakini watu wawe na masikio ya kusikiliza kitu. Sio watu wote wanaweza kufanana ya Diamond japokuwa kuna vitu tunaweza kufanana kwa sababu ni watu ambao tunakaa pamoja kwa muda mrefu. Pia watu wakiwa wanaishi muda mrefu pamoja huwa wanafanana, kwa hiyo kuna muda mkikaa pamoja kuna vitu mnaanza kushare lakini ukichunguza ndani yake kila mtu ana kitu chake,”

Mbowe aeleza mahusiano yake na Wema Sepetu

Freeman Mbowe ambaye ni kwenye kitu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu uhusiano wake na Wema Sepetu baada ya clip ya sauti inayosambaa mitandaoni.

Freeman amekana kutoka kimapenzi na kukana
clip hiyo. Kulingana na yeye hakuna kitu kinachoendelea Kati yake na Wema Sepetu. Akizungumza na kipindi cha XXL cha Clouds FM alisema,

“Kitu ambacho naweza kukisema kwa sasa hizo taarifa sio za kweli na timu yangu ya mtandao inajaribu kufuatilia kujua, na ukweli utajulikana muda sio mrefu.”

Hata hivyo alikataa kuzugumzia clip hiyo kwa kudai kuwa hawezi kusema nani alizindua audio hiyo…aliendelea kwa kusema

“Hapana yule ni kiongozi wa kijamii kwa maana kwamba ni mwanachama wetu aliyejiunga na chama chetu, na wapo wanawake, wasichana, wapo watu wengi kwenye chama chetu ni kwamba kuna mahusiano si kweli ni taarifa tu za upotoshaji.”

Huyu ndiye mrembo mpya anayetoka kimapenzi na Harmonize

Wikendi hii Harmonize kwa mara ya kwanza aliweka picha ya mpenzi wake mpya baada ya wengi kumchana kwa kumwaga Wolper.

Kama ilivyokuwa ikitangaza kwenye mitandaoni, Harmonize anatoka na mrembo wa kizungu na kama hiyo haijatosha wawili hao wanatarajia mtoto wao wa kwanza.

mambo haya mawili yamewaacha mashabiki kama wameduwaa kwa sababu mimba hiyo inaonekana kuwa ina miezi 6.

Hata hivyo, Wolper naye ameonekana aliendelea na maisha yake bila kujali kile mpenzi wake anafanya. Tazama picha hizo hapa;

Kuna nini Kati ya Vanessa Mdee na baby Madaha?

Msanii wa Bongo baby Madaha amedai kuwa kwenye industry ya bongo hakuna waimbaji wa kike ambao wanatalanta ya kuwafanya kuwania Tuzo za kimataifa.

Akizungumza na watangazaji wa Sibuka FM katika kipindi cha 180 Power, Byno na Joco, baby Madaha aliskika akimgusa Vanessa Mdee kwa kusema kuwa kunawaimbaji wa kike ambao hutajwa kuwania tuzo mbalimbali ilhali hawashindi hata moja.

Hata hivyo maneno yake yalionekana kumlenga vanessa ambaye nimsanii wa kike kutoka Tanzania ambaye amewania tuzo kadhaa. Baby Madaha alisema,

“Tunapeleka watu kuwania tuzo wengine hawana vigezo vya hizo tuzo, especially nazungumzia kwa madada kuna dada mmoja yaani kila tuzo anaendaga lakini ashindi kutokana na nini hana qualification za hizo tuzo,”

Huu ndio ujumbe ambao Harmorapa aliandika baada ya kupanda Ndege kwa mara ya kwanza

Harmorapa ni mmoja wa wasanii ambao hawakuwa na hella wala starehe kabla ya kuanza biashara ya muziki.

Kama msanii ambaye anaelewa shida za kutokuwa na hela, Harmorapa amekuwa mtu ambaye anajipanga ili asiziharibu hella zake na kwa sababu hii imemchukua muda kabla yeye kupanda ndege maishani mwake.

Hata hivyo hivi karibuni aliweka picha huku akiwa kwenye uwanja wa ndege. Kulingana na alichoandika, hii ndio ilikuwa Mara yake ya kwanza kupanda ndege na hangeweza kuificha furaha yake. Aliandika kusema…

“Maisha ni safari ndefu na mpangaji ni mwenyezi Mungu. Ukweli sikuwahi kuwaza katika maisha yangu kama ipo siku nitatimiza moja ya ndoto yangu ya kupanda ndege.
So ndugu zangu nawasihi ni mwiko kukata tamaa, omba Mungu sana atakutimizia ndoto zako. Shukrani #bossladySabuka kwa kunifikisha hapa nilipo, leo pia naomba Mungu ajalie aendelee kua na moyo huo wa kizungu maana kiukweli ni mzungu wa pekee.”

Ni bora Nikose Vyote Lakini Sio Wewe Mwanangu’ Rayvanny kwa mwanaye JayDanny

Msanii Rayvanny ambaye sasa ni baba,amemwandikia ujumbe mwanaye JayDanny.

Kupitia Instagram yake Ray anasema,’Mungu Akukukuze Mwanangu, Katika Mema na Mafanikio Katika Maisha Yako.Wewe Nifuraha Yangu Na pia Wewe Ndio sababu Ya Mimi kumwaga Jasho Nakufanya Kazi kwa Bidii Kila Siku. Ni bora Nikose Vyote Lakini Sio Wewe Mwanangu. I LOVE YOU SON @jaydanvanny ‘

Wakati huo huo mtoto Jay amekaribishwa rasmi kwenye Kundi la Wasafi na Diamond Platnumz,’Nikubalieni kumtambulisha rasmi star wetu mpya JayDanny,Mwana wa Ray Vanny. Karibu ulimwenguni!’

 

 

‘Allow me to introduce to you our brand new @wcb_wasafi Mega Star! JayDanny!!!! Mwana wa RayVanny!!!!! Welcome to the World Prince!! @jaydanvanny Cc @rayvanny ameandika Diamond.

Lizer amtaja msanii ambaye anafurahia kufanya kazi naye Wasafi

Muziki wowote wa Wasafi ukianza mara mingi utamsikia mwanadada akisema ‘ayo Lizer’ lakini wengine hawafahamu kuwa yeye ndiye mtayarishaji wa muziki kutoka studio ya Wasafi Records.

Hivi karibuni Lizer alimtaja msanii wa WCB ambaye yeye hufurai kufanya kazi naye. Akizungumza kwenye interview Lizer alisema kuwa Rayvanny ni msanii ambaye ameweza kufanya kazi naye bila matatizo yoyote.

Aliendelea kwa kusema,
“Msanii yoyote anayejua mimi nina enjoy sana kufanya naye kazi, ukimuelekeza fuata hiki anafuata. Lakini naweza kusema kwa kuwa Raymond ndiye msanii aliyegundua kitu kilichopo ndani ya Lizer huwa nina enjoy naye zaidi kwasababu ndiye msanii ambaye nilitoka naye.”

Ben Pol apata dili kubwa baada ya picha zake za Uchi

Msanii wa Tanzania Ben Pol aliwaacha wengi kama wameduwaa baada ya kuachia picha zake huku akionekana uchi. Kama kawaida mashabiki walimponda na wengi kumkashif kwa kuachia picha kama zile mitandaoni ya kijamii.

Hata hivyo msanii huyo sasa hivi amepata dili na kampuni ya mafuta ambayo imempa jukumu la balozi. Ben Pol alifunguka kuhusu dili hiyo alisema,

“Hapa sasa hivi tunaongea kuhusu majukumu yangu kama balozi, nione nina show ngapi katika hiyo event na mambo ya maslai inakuaje, anione matangazo ya runinga na mabango na nijue amount ya kazi yote ilivyo ni kiasi gani ninaweza kunufaika.Tukifikia muhafaka watu wataniona kwenye mabango, nimekoleza mafuta nimeweka na logo za hiyo kampuni,” 

Nandy ataja baadhi ya changamoto anazozipata kwenye muziki

Nandy ni msanii ambaye ameanza kutamba Tanzania kwa haraka. Hata hivyo kama wasanii wengine pia yeye a spirit changamoto ambazo ameweza kuzitaja kwenye Interview yake hivi karibuni.

Muimbaji huyu amesema kuwa kwa sasa anajaribu kuwapa mashabiki wake nyimbo ambazo wasanii wengine hawafanyi. Kulingana na yeye inampaswa awe na ubunifu ambao utaweza kumfungulia njia za kupenya Afrika Mashariki.

Aliendelea kwa kusema kuwa changamoto anazopata kwa sasa ni kushindana na wasanii wa kike ambao wamepenya kwenye muziki. Akizungumza naTBC Taifa Nandy alisema,

Nandy
Nandy

“Yaani nikija kutoa wimbo usishuke au uwe juu zaidi, au nifanye ubunifu gani kutofautiana na wenzangu ili niweze kubakia katika nafasi yangu. Wasichana wote kwenye industry wapo katika ushindani  kwa sababu tunafanya biashara moja, kwa hiyo ninapomuangalia mtu kama Maua namuangalia kwa jicho la kama msanii mwenzangu, kwa jicho la kibiashara, kwa hiyo namuangalia kama mshindani wangu.”

Vera Sidika asema atapata mtoto akiwa miaka 30

Mrembo kutoka Kenya, Vera Sidika amefunguka kwa Mara ya kwanza kudai kuwa anapanga kupata mtoto kabla ya kufikisha Miaka 30.

Ingawa hii sio Mara yake ya kwanza kudai kuwa anataka mtoto, Vera Sidika sema kuwa Ana mipango ya kupata mtoto kabla hajafikisha umri Wa Miaka 30 kwenye kipindi cha Talk Central. Aliendelea kusema kuwa hataki kupata mtoto akiwa mzee ili ajipe nafasi ya kuurudisha mapema umbo lake.

“I am getting a baby before I turn 30. I want to get a baby before I am too old then get my sexy body back. Sperm banks are here with us and there is nothing wrong with taking that route.”

Aliendelea kwa kusema,

“I am not the kind that believes in marriage. Honestly, I don‘t need a man to get a baby. I don’t think relationships are made for people like me. I have been proposed to twice, once by a very prominent personality but that is not my thing. Every time I try to date I stay like three months and it doesn‘t work so I kind of stopped going that emotional way. I mean, I don‘t want to have 100 divorces and be branded heartbreaker.”

Jarida la Forbes Africa la mtaja Jokate miongoni mwa vijana walio na umri chini ya miaka 30 wenye mafanikio mbalimbali mwaka 2017

Jokate ambaye amekuwa akijitahidi na mambo mbalimbali amejipata miongoni mwa watu ambao wametajwa na jarida la Forbes kumsheherekea kwa bidii yake.

Marafiki zake pia hawakuchelewa kwa kumpongeza dada huyu kupitia mitandao yao ya kijamii. Hata hivyo pia Jokate aliweza kuandika ujumbe kupitia Instagram yake kuwashukuru Forbes Africa kuonyesha furaha yake. Aliandika kusema,

“Looks whose on the cover of Forbes Africa with some other amazing young Africans doing amazing things to create wealth and transform our economies? God is so amazing. ???❤️?.”

Akaongeza kusema,

“Never underestimate your own strength. You were born for a purpose and are blessed with an ability to achieve it. Mpaka kieleweke ????”

Lava Lava afunguka kuhusu bosi wake wa Wasafi Records

Lava Lava ndiye msanii mpya kwenye label ya Wasafi Records na baada ya kuachia wimbo wake mpya bora Tuachane msanii huyo ameonyesha kuwa anatalanta ambayo itampeleka mbali.

Hata hivyo hivi karibuni akizungumza na Mzazi Willy M Tuva kwenye kipindi cha Radio Citizen, Lava Lava alisema kuwa ilimchukua muda wa mwaka mmoja kukutana na Diamond Platnumz macho kwa macho.

Kulingana na Lava Lava hii ilikuwa kama mtihani kwake kwa sababu kuna wakati akate tamaa. Alimwambia Willy

“Ilikuwa inanivunja moyo sana, kwamba sasa itakuwaje na ndoto zangu ni kumuona Diamond kwa sababu ni kioo chetu mtaani tunamuangalia nikaona kama itakuwa hanifuatilii kumbe yeye anafuatilia stori zangu sema ni katika kuniona kama nina moyo na uvumilivu,”

Wolper aeleza sababu za mahusiano yake kutodumu

Mapenzi ya Harmonize na Wolper yameisha kulingana na fununu zinazotambaa mitandaoni. Wawili hao wameachana kwa sasa na kulingana Wolper, yeye hana bahati kwenye mapenzi.

Akizungumza hivi karibuni Wolper alifunguka kwa kusema kuwa anakipaji cha kukomeshwa na wanaume wote ambao ametoka kimapenzi nao. Alisema,

“Mimi ni kama nina kipaji cha kukomeshwa kwenye mapenzi kwa sababu kipaji ninachokivumbua mimi wenzangu wanataka wapite hapo hapo ili kunikomoa. Ni kwamba nina kipaji cha kukomeshwa lakini huyo anayenikoa unakuta hajui mimi nimepambana vipi kumtengeneza mtu anipendae”

Hata hivyo Harmonize anasemekana kuwa anampenzi mpya ambaye ni mtoto wa Kizungu.

Diamond Platnumz aeleza sababu hataki Tiffah awemsanii kama yeye

Wasanii wengi duniani hawapendi kuwaonyesha Watoto wao mitandaoni na ukiwaukiza, hii ni kwa sababu wanahofia watoto wao kuishi maisha kama wanayoishi.

Mmoja wao ni Diamond Platnumz ambaye anahofia mwanawe, Tiffah Dangote kuwa msanii. Akizungumza kwenye mahojiano na Larry Madowo wa NTV Kenya Diamond alisema kuwa Tiffah akiwa msanii atatembea na wanaume wengi kitu ambacho yeye mwenyewe hataki kukiona ama kusikia. Alisema,

“Mtoto wangu wa kiume ningependa awe msanii lakini mtoto wangu wa kike sitaki awe msanii, watamla sana. Mtoto akiwa msanii watu wanaomjua wanakuwa wengi, watu wanaokujua wakiwa wengi na kutongozwa kunakuwa kwingi, sasa watanipa presha. Ukiwa mwanaume lijali na ukiwa kwenye nafasi kama yangu lazima wataliwa. Nilikuwa kwenye kutafuta tafuta, mpaka nilivyompata Zari na kweli nimetulia,”

Tazama interview hiyo hapa:

“It hurts to think that you are not here” huu ndio ujumbe ambao Raphael alimwandikia baba yake Ivan Don

Familia ya Zari Hassan inaomboleza kifo cha Ivan Don aliyefariki Jumanne baada ya kuugua kwa maradhi ya moyo.

Zari alimwandikia Ivan ujumbe huku akiomboleza kifo chake na pia kumsheherekea kwa kuwa mfano mzuri kwa Watoto wake muda wote aliokuwa hai.

Hata hivyo Raphael ambaye ni mmoja wa watoto wa Ivan aliandika ujumbe kwenye Instagram yake huku akimuomboleza babake ambaye kwa sasa amewaondokea wakiwa bado wadogo. Raph aliendika kusema,

“It hurts to think that you are not here anymore. Although I can’t help but smile with tears in my eyes to think of how we cherished each and every moment of our lives together; I will miss you Dady and I cant stop crying anymore when i think of you Dady @ivandon may your souls rest in peace.”


Mungu aiweke roho yake pahali Pema.

Ni kweli kuwa aliyekuwa mpenzi wa Zari, Ivan Don alitiliwa sumu kwenye chakula?

Fununu mitandaoni inadai kuwa Marehemu Ivan Don alifariki baada ya kutiliwa sumu chakulani chake pale ambapo alikuwa akikula na marafiki wake wa Karibu.

Ripoti hizi zilisambazwa na gazeti moja la Uganda liloandika kudai kuwa kuna ushahidi wa maneno haya. Hata hivyo kulingana na tulichoambiwa na familia yake ni kuwa Ivan Don alifariki baada ya viungo vyake vya mwili vilipoanza kufaili kwa kuwa alikuwa anapumua kupitia usaidizi wa machine.

Familia yake imenyamaza na hakuna aliyechangia kwenye ripoti za Ivan Don kupewa sumu na adui yake ambaye ni mmoja wa marafiki wake wa karibu.

Gazeti hilo liliandika kusema,