“Sio mbaya mkiniita Gigy Dangote” Gigy aeleza anavyompenda Diamond Platnumz

Gigy Money ambaye ni video vixen mkubwa kutoka Tanzania amewaacha wengi wakijiuliza uhusiano wake na Diamond Platnumz ni upi baada ya yeye kuweka picha yake akiwa na CEO huyo wa Wasafi records huku akiandika kusema anavyompenda.

Mwana dada huyu ambaye amefanya kazi na wasanii kama Harmonize hata hivyo hakuwa na nafasi ya kuwajibu mashabiki wake ambai walitaka kujua kama alikuwa anammezea msanii huyu.

Kupitia mtandao wake wa Instagram, Gigy aliandika kusema…

Nampenda sana Chibu sio kwamba ajui ?ila sio mbaya mkiniita gigy dangote❤ amen? #ilatunapendezana @diamondplatnumz

Mashabiki wengine waliacha majibu ya kumponda mrembo huyu wakimfananisha na Zari Hassan huku wengine wakimwabia mtu anayemfaa sana ni Harmorapa. Tazama picha hiyo hapa chini.

Tunda aeleza kwanini hatoweka mambo ya mapenzi yake kwenye mitandaoni kama zamani

Mrembo Tunda ambaye anajulikana kutokea kwenye video za wasanii wakubwa wa bongo amefunga kusema kuwa kwa hivi sasa hatamani mapenzi ya mitandaoni. Hapo mbeleni alikuwa akitoka kimapenzi na Young D lakini baada ya mambo kadhaa wawili hawa waliachana na kila mmoja kwenda njia yake.

Tunda
Tunda

Akizungumza na Uwazi Showbiz hivi karibuni mrembo huyu alisema kuwa uhusiano wake na Young D ulikuwa sana mitandaoni kitu ambacho hakuwa anajua inaweza kuleta utata.

Hata hivyo kulingana na yeye, hatorudi kufanya hivi tena kwa sababu amejua kuwa sio marafiki wake wote wanamtakia mazuri na badala ya kumueka mpenzi wake mitandaoni anaonelea kukaa kimya. Alisema,

“Kiukweli nimejifunza juu ya kuwa muwazi katika suala zima la mapenzi kuwa kuna watu wengine hawapendi kuona mnakuwa na furaha.Hawa huweza kupenyeza maneno ya kuwagombanisha ilimradi tu muweze kuachana, sasa mimi nimeamua katika uhusiano wangu wa sasa kutokuwa muwazi, mtu anayefahamu juu ya ninatoka na nani kwa sasa lazima atakuwa amefanya kazi ya ziada.”

Je Harmorapa nimkali kuvaa kumshinda Dogo Janja?

Inaonekana Harmorapa anafurahia kuandikwa kwenye magazeti kila kichao. Kila wakati msanii huyu kutoka bongo ako kwenye mitandaoni kutafuta kiki lakini kwa sababu inamsaidia kupata pesa, basi Harmorapa hatawacha hadi afike anapotaka.

Wakati huu, Harmorapa ameamua kumuingilia Dogo Janja kwa kusema msanii huyu hawezi kuvaa vizuri kama yeye. Kulingana na Harmorapa kuwa yeye huvaa nguo kali kitu ambacho Dogo hawezi fikia.

Dogo Janja
Dogo Janja

Akizungumza kwenye interview Harmorapa alisema,

“Dogo Janja asijinadi sana kwenye kuvaa, mwambie tupo wanyamwezi kama sisi tunavaa pamba kali. Najua na yeye ni mkali wa kuvaa lakini mimi ni mkali zaidi kwenye hizo, kwanza angalia jinsi nilivyotupia leo, kinyamwezi,”

Harmorapa aliendelea kwa kudai kuwa Dogo Janja bado ni mtoto mkubwa mbaye anajaribu kufanya msmbo ya watu wakubwa.

“Mimi simtaki Naseeb tena!” Wema Sepetu amwambia shabiki wake Instagram

Japo ni wengi bado hutarajia Wema Sepetu na Diamond Platnumz kurudiana, mrembo huyu ameweka wazi kuwa hamtamani Diamond tena na mapenzi yao yalikwisha kitambo sana.

Wema Sepetu alisema haya baada ya mmoja wa mashabiki wake aliandika kumuuliza iwapo ameshindwa kumpata Diamond Platnumz kupitia Instagram. Shabiki huyo aliandika kusema,

Wema Kwa uzuri huo umeshindwa kumkamata Diamond mpaka anakupa mawazo wanaume hawana lolote jitahidi

 

Kupitia tu Instagram Wema pia yeye alimpa shahidi huyo jibu ambalo lilidhibitisha kuwa mrembo huyu ameyaacha maisha yake ya kitambo na hivi sasa anatarajia mwanaume ambaye atamchukua alivyo. Wema aliandika kusema,

@Veronikakihonga Sasa baby alokwambia mi namtaka Diamond ni nani…?Life has to go on… Yule ni baba wa watoto wawili Jamani… Its about time u guys accept that me and Naseeb are no more. Mnachotakiwa ni kuniombua ni nipate mwanaume Bora na sio Bora mwanaume…Mwenye heshima zake tena ambaye hata haijulikani…Kajisemea dada angu @mangekimambi…mwenye hela miiingi

Harmonize apiga show nyumbani kwao Mtwara, hivi ndivyo mashabiki walijitokeza (Picha)

Iwapo kuna msanii ambaye anatambulika Afrika Mashariki ni Harmonize. Hii ni kwa sababu ni mmoja wa wasanii kutoka WCB na pia kwa sababu ya mchumba wake anayetambulika kwenye muvi za bongo, Wolper.

Hata hivyo weekend hii Harmonize alijiunga na wasanii wengine kupiga show nyumbani kwao Mtwara. Mbali na show hii yake msanii huyu alikuwa amepanga kutembelea Hospitali ya Mkoa kuwaona wagonjwa na pia kuwasaidia baadhi ya wale ambao walikuwa wanahitaji fedha.

Kulingana na picha zilizochukuliwa katika show hiyo, inaonekana kuwa Harmonize alikuwa amewavutia wengi na ingawa Young Killer, Shilole na Aunty Ezekeli walikuwepo… mashabiki hawa walimtambua Harmonize zaidi.

Tazama picha hizo hapa.

“Akumbuke alianzia chini mpaka kufika alipo sasa” Harmorapa amjibu Afande Sele

Kwa sasa hakuna mtu ambaye hamjui Harmorapa kutoka Tanzania. Rapa huyu amekuwa kwenye mitandao kadhaa na wengi hupenda kuongelea nyimbo zake lakini Afande Sele hivi karibuni alidai kuwa hakuwa anamjua Harmorapa hadi liletokeo la Nape kushikiwa Bastola.

Afande Sele
Afande Sele

Maneno haya yanaonekana kuwa yalimuudhi muimbaji huyu ambaye amefunguka kupitia mahojiano yake na EATV. Harmorapa alisema kuwa yeye hana maneno mengi ya kusema lakini kwa sasa Afande Sele anapaswa kujua kuwa hakuna mtu anayeanzia juu kwani pia yeye alianzia chini ndipo afike alipo sasa.

“Niseme tuu yeye kwanza mwenyewe akae chini na kujua na kukumbuka kuwa alianzia chini mpaka kufika level fulani watu wakamkubali.”

Aliendelea kusema,

“Ajue mimi kama Harmorapa sina maneno mengi ila kazi zangu ndiyo zitakuja kumuelekeza kuwa Harmorapa uliyekuwa unamuongelea ndiyo huyu kupitia kazi yangu ndiyo itakuwa imemnyoosha au vipi? na ku’prove ukali wa Harmorapa.”

Wema Sepetu na Diamond Platnumz washerekea pamoja katika party ya Sallam

Waliokuwa wapenzi Diamond Platnumz na Wema Sepetu jana uikutana katika sherehe ya kuzaliwa ya Meneja wa Diamond Sallam Sharaff.

Sherehe hii ambayo ilifanyika Castle Lite iliwavutia wasanii kadhaa ambao walijitokeza kama wamevaa mavazi ya kizamani huku ikiwakutanisha Wema na Diamond Platnumz.

Ingawa wawili hawa hawajaonekana wakiwa pamoja katika picha ambazo zinasambaa mitandaoni, wengi wameachwa wakijiuliza ikiwa walipata nafasi ya kuongea kwani hii ndio mara ya kwanza kwa wiwili hawa kuwa katika sherehe moja tangu kuachana mwaka wa 2015.

Hata hivyo Wema Sepetu alionekana kurembeka kwa mavazi yake na mapambo yake ya kawaida.Tazama picha yake hapa.

Wema Sepetu katika party ya Mendez

Baada ya Diamond Platnumz kuzindua perfume yake, King Kiba kuingiza bidhaa moto moto sokoni

Japo King Kiba amekuwa kimya kwa muda sasa msanii huyo amefunguka na kusema kuwa sasa hivi anajiandaa kuachia bidhaa kadhaa kutoka kwa AK na sasa King Kiba.

Ali Kiba

Kwa sasa muimbaji huyo wa Aje ameachia shati na kofia ambazo zimekuwa zikiuzwa Afrika Mashariki. Lakini kwa sasa anatarajia kuachia viatu, glasses na energy drink. Alisema haya kupitia kipindi cha XXL cha Clouds FM.

“AK ni brand ya Alikiba nashukuru imekuwa kubwa watu wanavaa lakini pia ipo na ya King Kiba nayo ni brand yangu na zipo official kabisa na kazi zitakapoanza watapata product zote.”

Aliongeza kwa kusema kuwa anamalengo makubwa na ndio maana bidhaa zake zinachukua muda kuachiliwa sokoni.

“Kuna malengo makubwa sana tumeyaweka lakini siwezi kusema sasa hivi ila kuna jeans, viatu na glasses tayari zishatoka soon wataziona maana hizi zitakuwa za kwanza sababu tayari zishatoka na kuna energy drink”

Mama yake Lulu Elizabeth Micheal adai kuwa hataki kutajiwa mambo na harusi ya mwanae tena

Mama Lulu, Lucresia Karugila amedai kuwa hataki waandishi wa habari kushinda wakimsumbua na suala la ndoa ya mwanae. Mama huyu ambaye hakuoneka kuwa na furaha alisema haya baada ya mwandishi mmoja wa Global publishers kujaribu kujua kikao cha harusi hiyo kimefika wapi.

Mama Lulu

Lucresia Karugila anasemekana kuwa alidai kuwa hana kitu cha kusema kuhusiana na ndoa ya lulu kwani hakuna anayetaarifa za kudhibitisha kuwa mwanae anaoleka na alikyekuwa mpenzi wa Hamisa Mobeto, Majay.

Mama huyo aliendelea kudai kuwa amechoswa na suala hili na kwa sasa hataki kuhusishwa na mambo ya kijinga. Mazungumzo yake na mwandishi huyo yalienda hivi.

Amani: Mama nataka kujua nini kinaendelea kwenye vikao vya mwisho vya harusi ya Lulu na ….(akitajiwa jina
la mchumba wa Lulu), wewe kama mama unasemaje?

Mama Lulu: Sitaki kabisa, kwanza una mama wewe? Sitaki kusikia ukinifuatilia na nilishakuambia tangu zamani, sitaki uniulize mambo ya kijinga kama hayo, hayanihusu kwa vyovyote, tena nisikusikie
kabisa, niache nifanye mambo yangu ya msingi, unasikia? Achana na mimi, tiiiii….titiiiiii (akakata simu).
Jitihada za kumpata Lulu kwa lengo la ufafanuzi juu ya jambo hilo la heri ziligonga mwamba kufuatia simu yake kutokuwa hewani hivyo jitihada bado zinaendelea.

Huu ndio ujumbe Diamond Platnumz amemwandikia professor Jay kupitia Instagram

Diamond Platnumz amewaacha wengi wakishangaa baada ya ujumbe aliomwandikia mbunge wa Mikumi Joseph Haule a.k.a Prof Jay. Msanii huyo wa Wasafi records aliandika kumwambia Prof Jay sababu ambazo yeye hakujitolea kutumbuiza kwenye kampeni zake mwaka uliopita.

Hit maker wa Marry me aliandika kusema,

“Ndio Maana kwenye Jimbo lako sikuja kupiga kampeni bro…kwakuwa niliijua mapema thamani na umuhimu wa Uwepo wako kwenye hilo jengo….. @professorjaytz

Hata hivyo wengi wasichokielewa ni kwa nini msanii huyo alimchana mwenzake ata baada ya yeye kumshughulikia bungeni baada ya kudaiwa kuwa anadeni la TRA la milioni 400.

Wasanii wengine hata hivyo wamekuwa wakimuunga mkono Prof Jay ambaye anawashungulikia wasanii kwani pia yeye anaelewa shida ambazo wao hupitia.

Aliyekuwa meneja wa Young Dee adai kuwa msanii huyu amerudia kutumia madawa ya kulevya

Young Dee amejipata matatani baada ya Max Rioba aliyekuwa meneja wake kupitia label ya MDB kusema kuwa msanii huyu amerudia madawa ya kulevya na kuwa hana bidii kwenye kazi yake tena.

Max alifunguka kusema haya baada ya Young Dee kudai kuwa alimtoroka meneja huyu baada ya kujua kuwa alitoka na mrembo wake, Tunda. Hata hivyo Max amedai kuwa msanii huyu wa bongo amepoteza muelekeo wake kama anaweza kusingizia kuwa alitoka na Tunda ilhali anajua kilichofanya wawili hawa kuacha kufanya kazi pamoja.

Young Dee na aliyekuwa meneja wake, Max

Akizungumza kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM Maz alisema,

“Mimi sikuwahi kumfukuza huyo mtoto kwaajili ya Tunda. “Nimemfukuza sababu ya matumizi yake ya dawa za kulevya na utovu ya nidhamu na ujinga ujinga wake. Kwani mara ngapi Tunda amekuwa na Dee tukiwa naye hapa, yeye Dee kasema ni moja kati ya sababu za kuondoka hapa, sio kweli sina chochote na huyo mtoto,”

Max aliendelea kwa kusema,

“Nachojua ni kwamba ana wakati mgumu sana kwenye game, industry imebadilika, kuna watoto wamekuja wanafanya vizuri, ndio maana anaendelea kusema Dimaond hawezi kushuka kwa sababu anajijua anachofanya, Dee hana heshima na nidhamu kwenye kazi hana.”

Nandy adai wanaume wengi wamekuwa wakihaha kutaka kuonja penzi lake

Faustina Charles anaejulikana kama Nandy ni mwanamziki kutoka bongo na ukimuangalia, yeye ni msichana ambaye anawazingua wanaume wengi. Sio kwa rangi yake pekee lakini pia kwa sauti yake ambayo inaweza kumtoa nyoka pangoni.

Akiznungumza na Za Motomoto News, Nandy alikiri kuwa kwa sasa kuna wanaume kadhaa ambao wamekuwa wakimsumbua. Tangua kuachia wimbo na Chege – Nandy anasema kuwa hajapata amani ata hivyo hicho ni kitu ambacho wengi walitarajia kwani ni mrembo kupindukia.

Nandy
Nandy

Hata hivyo Nandy amesema kuwa hana mpango wa kuwataja wanaume hawa lakini wengi wao wanatamani sana kuonja penzi lake. Alisema,

“Usumbufu ni mkubwa mno kwa kweli, lakini siwezi kuwataja majina hata hao vigogo wanaonisumbua, mimi ni msichana ninayejielewa na wanaume wengi wamekuwa wakihaha kutaka kuonja penzi langu, wanagonga mwamba.”

“Siwezi kumfurahisha kila mtu” Linah awajibu wanaotaka afunike tumbo lake

Linah ambaye anamtarajia mtoto wake wa kwanza hivi karibuni ameamua kuwajibu mashabiki ambao wameonesha kuwa na shida na picha ambazo aliweka kwenye mtandao wake wa Instagram kuonesha tumbo lake.

Msanii huyu wa Bongo alisema haya baada ya mashabiki kadhaa kuacha maoni ambayo yalikuwa ya kuudhi kwenye picha zake ambazo aliweza kuonesha ujauzito wake.

Linah aonesha Ujauzito wake
Linah aonesha Ujauzito wake

Hata hivyo Linah haoni ubaya wa picha hizi na ndio maana amewajibu mashabiki hawa. Kulingana na alichosema, Linah haoni kwamba anaweza kufurahisha kila mtu na kwa upande wake haoni kama kuna shida yoyote.

“Siwezi kumfurahisha kila mmoja ndio maana anafanya kile ambacho anahisi kipo sahihi kwa upande wangu pia wakosoaji wapo wengi tu”

Huyu ndiye mrembo mpya wa Harmorapa? (Picha)

Kuna uvumi kuwa Harmorapa amepata mrembo mpya ambaye amewaacha wengi wameduwaa kwa muonekano wake.

Harmorapa
Harmorapa

Harmorapa ambaye anajulikana kupenda kiki hata hivyo hajazungumzia jambo hili kwani kwa sasa anajitahidi kusambaza wimbo wake mpya, Nundu aliyoiwachia jana.

Kulingana na picha ambazo zinasambaa mitandaoni rappa huyu wa Bongo amekuwa akionekana na mrembo huyu kitu ambacho kimewafanya wengi kumfikiria kuwa wanatoka pamoja.

Hata hivyo sio siri kuwa rapa huyu anakimbizwa na wanawake ambao wanatamani maisha yake ya sasa. Angalia picha ya mrembo huyo akiwa na Harmorapa hapa:

Harmorapa
Harmorapa

Diamond Platnumz adaiwa kodi ya zaidi ya Sh. milioni 400

Hitmaker wa Nasema Nawe Diamond Platnumz amejipata kwenye matata baadaya mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia kudai kuwa msanii huyo anadeni la Sh. milioni 400 analodaiwa na Mamlaka ya Mapato (TRA).

Akizungumza bungeni Maulid Mtulia aliweka wazi kuwa msanii huyu amekuwa akikwepa kulipa TRA kitu ambacho wasanii wakubwa kama yeye hufanya. Mazungumzo haya yalifanyika bungeni wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Diamond Platnumz anadaiwa pesa hizi kwani yeye ni mmoja wa wasanii ambao wanaoingiza pesa nyingi kupitia nyimbo zake lakini inaonekana muimbaji huyo amekuwa akikwepa kupeana pesa hizi kama inavyohitajika kila mwezi.

Hata hivyo Diamond Platnumz hajazungumzia swala hili ambalo limewaacha Watanzania kama wameshangaa.

Darassa aeleza sababu za ‘Hasara Roho’ kutofanya vizuri kama ‘Muziki’

Muimbaji Darassa hivi karibuni aliachilia wimbo wake mpya ‘Hasara Roho’ lakini inaonekana kuwa mashabiki wake hawajaupokea kama wengi waliovyotarajia.

Ingawa wimbo huu hauna tofauti kubwa na Muziki sio wengi wameonyesha kuupenda na pia haujapata mtamzamo mkubwa kupitia YouTube.

Hata hivyo akizungumza kupitia kipindi cha 255 XXL cha Clouds FM, Darassa alisema kuwa mashabiki wake wamezoea Muziki zaidi kwa kuwa alikawia kuwachilia project mpya.

“Kitu ambacho kinatokea ni wimbo wa muziki umewakaa sana na kuusikiliza sana kwa namna moja au nyingine.”

Aliendelea kusema kosa lao ni kumtegemea kuachia wimbo kama Muziki ambacho hangeweza kufanya kwani kila anapoachia nyimbo lazima iwe tofauti.

“Mimi mwenyewe nilikaa sana na huu wimbo na kuupima, nikaona kuwa ni project ambayo inafaa kufuata na ikawatosha. Kwa hiyo kwa watu kukaa na kutegemea kuwa uje wimbo kama “Muziki” hiko ndio kitu kinachorudisha sanaa yetu nyuma.”